Tuesday, 16 August 2016

USIKU WA HARUSI (NDOA)

Unknown

Mlango 1: Usiku Wa Harusi (Ndoa)

A’mali Za Usiku Wa Harusi




 Imesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w) kwamba:Milango ya Peponi kwa ajili ya rehema itafunguliwa katika hali nne: Wakati inaponyesha mvua; wakati mtoto anapoangalia kwa huruma usoni kwa mzazi wake; pale mlango wa Ka’ba unapokuwa wazi, na wakati wa (kutokea) harusi.
Kama inavyoonyeshwa na hadithi hiyo hapo juu, dhana ya harusi katika Uislam ni tukufu mno na yenye kuthaminiwa, kiasi kwamba milango ya rehema ya Mwenyezi Mungu inafunguliwa katika tukio hili.
Naam, hili halishangazi pale mtu anapochukulia kwamba ndoa inahifadhi sehemu kubwa ya imani ya mtu na kuilinda na uovu wa Shetani, kama ilivyosimuliwa kutoka kwa Mtume (s.a.w):

 “Hakuna kijana yeyote atakayefunga ndoa katika ujana wake, isipokuwa kwamba shetani wake anapiga makelele akisema: ‘Ole wake, ole wake, amezikinga sehemu mbili ya tatu ya imani yake kutokana na mimi;’ 

kwa hiyo mwanadamu lazima awe na taqwa (mwenye kumcha Mungu) kwa Mwenyezi Mungu ili kulinda sehemu moja ya tatu ya imani yake iliyobakia.
Ni muhimu kwa hiyo, kwamba wawili hao, pale wanapoingia kwenye hatua hii, wachukue hadhari ya hali ya juu kulinda usafi wa muungano huu mtukufu na wala wasiutie doa tangu mwanzoni mwake kwa kuruhusu lile tukio la sherehe ya harusi kuwa ni chanzo cha madhambi na israaf.
Hususan ule usiku wa harusi ndio usiku wa kwanza ambao mwanaume na mwanamke wanakuja pamoja kama mume na mke, na imekokotezwa sana kwamba wanaunda muungano huo kwa nia ya kupata ukaribu na radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu na kufanya zile A’amali zilizopendekezwa kwa ajili ya usiku huo.
Wakati huu ni muhimu kuangalia ni hali gani yule ‘Bibi wa wanawake wote wa ulimwengu,’ Hadhrat Fatimah (a.s.) aliyokuwa nayo ule usiku wa harusi yake, na ni vipi alianza maisha yake na mume wake, Imam Ali (a.s.): Katika ule usiku wa harusi Imam Ali (a.s.) alimuona Hadhrat Fatimah (a.s.) alikuwa amefadhaika na akitokwa na machozi, na akamuuliza kwa nini alikuwa kwenye hali ile.
Yeye alijibu akasema: “Nilifikiria kuhusu hali yangu na vitendo na nikakumbuka mwisho wa uhai na kaburi langu; kwamba leo nimeondoka nyumbani kwa baba yangu kuja nyumbani kwako, na siku nyingine nitaondoka hapa kwenda kaburini na Siku ya Kiyama.
Kwa hiyo, namuapia Mungu juu yako; njoo tusimame kwa ajili ya swala ili kwamba tuweze kumuabudu Mwenyezi Mungu pamoja katika usiku huu.

A’amali Zifuatazo Zinapendekezwa Kwa Ajili Ya Usiku Huu

A’amali Zifuatazo Zinapendekezwa Kwa Ajili Ya Usiku Huu

1.  Jaribu kuwa katika Udhuu kwa kiasi kirefu kinachowezekana cha usiku huo, na                  hususan wakati wa A’amal zifuatazo hapa chini.
2.   Anza kwa kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu halafu useme “Allahu Akbar,”                    ikifuatiwa na Swala ya Mtume – Allahumma swali ‘alaa Muhammadin wa aali                         Muhammad).
3.  Swali rakaa mbili, kwa nia ya ‘Mustahab Qurbatan ilallah’ – kujisogeza karibu na                 Allah (s.w.t.). (Swala inayopendekezwa kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi                    Mungu) ikufuatiwa na Swala
       ya Mtume.
4.  Soma Dua ifuatayo, ikifuatiwa na Swala ya Mtume. Kwanza bwana harusi aanze                  kuisoma, baada yake ambapo bibi harusi atapaswa kusema: Ilahi Amin (Mwenyezi            Mungu aitakabalie Dua hii).
Allahumma rzuqniy ilfahaa wa wudhahaa wa ridhwaahaa wa radhwiniy bihaa thumma j’ma’u bayinanaa bi-ahsani j’timaa’in wa asarri itilaafin fainnaka tuhibbul-halaala wa takrahul-haraam.”
Ewe Allah! Nijaalie na upendo wake, mapenzi na kunikubali kwake mimi; na nifanye mimi niridhike naye, na tuweke pamoja katika namna bora ya muungano na katika muafaka kamilifu, hakika Wewe unapenda mambo ya halali na unachukia yale ya haram.”

5.  Hata kama wawili hao hawadhamirii kushika mimba katika usiku huo wa harusi,               inapendekezwa kwamba Dua zifuatazo zisomwe kwa ajili ya watoto wazuri (wakati          wowote itakapotunga mimba):

a. Bwana harusi anapaswa aweke kiganja cha mkono wake wa kulia kwenye paji la uso      la bibi harusi kwa kuelekea Qibla na asome:
Allahumma bi-amaanatika akhadhtuhaa wa bikalimaatika stahlaltuhaa fain qadhwayta liy minhaa waladaan faaj’alhu mubaarakaan taqiyyan minshiy’ati aali Muhammad wa laa taj’al lil-shaytwaani fiyhi shirkaan wa laa naswiybaan.
Ewe Allah! Nimemchukua (binti) huyu kama amana Yako na nimemfanya halali juu yangu mwenyewe kwa maneno Yako. Kwa hiyo, kama umenikadiria mtoto kutokana naye, basi mfanye mbarikiwa na mchamungu kutoka miongoni mwa wafusi wa familia ya Muhammad; na usimfanye Shetani kuwa na sehemu yoyote ndani yake.”

b. Dua ifuatayo pia inapaswa kusomwa:
“Allahumma bi-kalimaatika stahlaltuhaa wa bi-amaanatika akhadhtuhaa. Allahumma-j’alhaa waluwdaan waduwdaan laa tafraku taakulu mimmaa raaha wa laa tas-alu ‘ammaa saraha.”
Ewe Allah! Nimemfanya awe halali juu yangu kwa maneno Yako, na nimemchukua katika amana Yako. Ewe Allah! Mjaalie awe mwenye kuzaa na mwenye upendo.”

6.  Bwana harusi aioshe miguu ya bibi harusi na anyunyize maji hayo katika pembe               zote nne za chumba na nyumba. Mwenyezi Mungu Mtukufu ataondoa aina 70,000 za       umasikini, aina 70,000 za neema zitaingia ndani ya nyumba hiyo na neema 70,000           zitakuja juu ya bibi na bwana harusi. Bibi harusi atakuwa salama kutokana na                     wendawazimu, vidonda vya tumbo na ukoma.

Baadhi Ya Mambo Kwa Ajili Ya Bibi Na Bwana Harusi

1. Sio lazima kwamba kujamiiana kwa kutimiza ndoa kufanyike katika ule usiku wa              harusi; bali unaweza kuchukua siku chache au hata majuma machache.
2. Uchovu, wasiwasi na fadhaa vinaweza kufanya hilo liwe gumu zaidi; hivyo ni muhimu     kwamba mume na mke wachukue muda wa kutosha kuweza kuwa wametulizana na       kuzoeana na kwenda kwa mwendo wao wenyewe.
3. Mafuta ya kulainishia yanaweza yakahitajika kwa siku zile chache za mwanzo au                majuma ili kufanya kule kujamiiana kuwa rahisi zaidi na kwenye starehe zaidi.
4. Kumaliza mapema au kusikotarajiwa kunaweza kuwa ni tatizo kwa mara chache za          mwanzoni; hata hivyo, hili linapaswa kutatuliwa baada ya kupita muda na                            kupatikana uzoefu.
5. Kizinda (cha bikra) kinaweza kivuje au kisivuje damu. Unyegereshano, upole  na               kuingiliana tena mara tu baada ya hapo kunaweza kupunguza maumivu ya                          uchanikaji wa hicho kizinda.
6. Baada ya kujamiiana (wakati wowote itakapokuwa), bibi harusi asije akatumia                 maziwa, siki, giligilani, tuhafa chungu au tikitimaji kwa kiasi cha juma moja, kwani           vinasababisha tumbo la uzazi kukauka na kuwa la baridi na gumba. Kula siki wakati       huu vilevile kunatokezea kwa mwanamke kutokuwa msafi (tohara) kutokana na               damu ya hedhi, giligilani (na tikitimaji) kunasababisha matatizo ya wakati wa                     uchungu na tuhafa linasababisha kusimamisha ukawaida wa hedhi, na yote haya             yanaishia kwenye kuleta maradhi.
7. Watu wanaweza wakatoa maoni fulani juu ya siku chache zinazofuatia. Ni muhimu          sana kufanya hilo lisikuathiri wewe, na usivutike kwenye mazungumzo yao.
8. Usizungumze kuhusu mambo yako ya ndani kwa watu wa nje, chunga heshima kwa        mwenza wako na kwenye uhusiano wenu.


Unknown / Author & Editor

0 comments:

Post a Comment

Coprights @ 2016,