QADARI (KHERI AU SHARI INATOKANA NA ALLAH
(S.W))
.TUSIMLAUMU ALLAH.
Kama kila kitu kinatokana na Allah (S.W) atakavyopenda .
Yako wapi majaribu ? ( Then where is the test? )
Inamaanisha kwamba kila kitu kilishapangwa, ni kitu ambacho
kiko tayari ambacho kimeshaandikwa. Hakuna ambacho utafanya ila kitakuwa
kimeshapangwa kwa ajili yako.
Kumini Qadar (kheri au shari inatokana na Allah(S.W)) ni kitu
cha muhimu katika uislamu na ni miongoni mwa nguzo sita za Imani katika uislamu
ambazo muislamu anatakiwa kuamini.
VIPI TUNAWEZA KUAMINI QADARI ?
Ili kuelewa Qadari inatakiwa kuelewa mambo manne (4) ya
muhimu ili tupate kuelewa Qadar. Mambo hayo manne ni kama yafuatavyo :
1.
ALLAH S.W)
ANAJUA KILA KITU.
Allah(S.W) anajua kila kitu katika
wakati uliopita,uliopo na unaokuja. Hii inaonyesha kwamba Allah anajua kila
kitu. Katika Quran tukufu Allah (S.W) anasema:
( Na ALLAH ndiye ufunguo kwa yale
yasiyoonekana,Hakuna ayemiliki,Hakuna anayejua kuhusu hayo( Ila Allah (S.W)) na
anjua kila kitu katika ardhi na bahari, na hakuna jani linaloanguka ila anajua
kuhusu hilo jani, na hakuna mbegu inayoota kwenye giza ila anajua kuhusu hilo,
na hakuna kilicho kikavu au kibichi katika ardhi ila tayari kishaandikwa katika
kitabu.)
Kwa hiyo elimu ya ALLAH (S.W) ni
kwamba anajua kila kitu.
Na katika surat Bakara katika Ayatul
Qurusiyu Allah anasema:
( Anajua
yaliyopo katika mikono yao (ambayo tunayaona
sasa) na ambayo yako nyuma yao (ambayo hatuyajui yanayokuja) )
2.
ALLAH (S.W)
AMEEKA TUAMUE WENYEWE KATIKA QADARI ZETU.
Tunajua kwamba Allah SW anajua kila kitu kutokea mwanzo hadi mwisho,vinavyooneka
na visivyo onekana. Tunaposema elimu yake inajua kila kitu ni kwamba anajua maamuzi
yetu pia.
Pale unapochagua kufanya hiki ama
kile, ni chaguo hilo, lakini Allah(S.W) anajua maamuzi utakayoyafanya mbele ya mda.
Kwa hiyo unachagua maamuzi yako
mwenyewe katika Qadari yako. Allah (S.W) ,tumepewa maamuzi ya kuamua kufanya
hili ama lile kutoka na akili tulizopewa na Allah(S.W)
3.
ALLAH SW
AMETUPA MUONGOZO NA NGUVU ZA AKILI
Haujui Qadari (destiny) yako ila
Allah amekupa muongozo. Muongozo ambao ni Quran na Sunnah lakini sio hicho peke
yake ila amekupa na akili pia. Akili ambayo inaweza kufanya maamuzi sahihi
katika kuendea mema au maovu.
Kwa hiyo ukifanya maovu ni kosa lako
mwenyewe .
4.
HATUWEZI
KUBADILISHA QADAR ILA TUNAKUWA NA MAAMUZI
Kwetu sisi ni ngumu kubadilisha hivi
vitu ila tunaweza kuchagua na kufanya maamuzi sahihi katika yaliyo mengi juu
hili jambo.
Unafanya maamuzi mfano kuchagua X au Y unachagua, 1 au 2
unachagua, A au B unachagua. Lakini hatuwezi kubadilisha ila tunaweza kuchagua
tu.
Mfano useme kesho ntaamka ntaenda
kazini nitapanda gari au daladala au pikipiki ila hujui kama kweli kesho utaenda kazini na
utapanda gari au pikipiki au daladala . Maana huwezi kama usafiri kesho
utakuwepo, inaweza ikanyesha mvua kubwa ikashindikana kupata usafiri au usafiri
usiwepo na unaweza ukalala siku nzima na ukachelewa kuamka, PIA unaweza usiamke ukawa umefariki.
Kutokana na maaumuzi tutapata faida
au adhabu mbele ya Allah(S.W)
Majaribu yanaangalia kutokana na
maamuzi tutakayofanya na Qadari (Kheri au Shari). Peke yake Allah ndiye
anayeweza kubadilisha Qadar(Kheri au Shari).
Mara nyingine ALLAH anabadilisha
Qadari ya Shari kuwa Kheri kutokana na nia nzuri. Na pia Qadari ya Shari yaweza
kuwa Kheri tukifanya Dua. Ambayo pia ni kwenye nia njema.
ALLAH AMEKUUMBA NA AMEKUPA UWEZO WA
KUCHAGUA.
CHAGUA SASA
0 comments:
Post a Comment