Hakuna alama rasmi ambayo inatambulisha uislamu. Lakini kuna
alama nyingi ambazo zina nafasi katika Uislamu.
ALAMA YA NYOTA NA
MWEZI
Alama(ishara)
ya nyota na mwezi ni alama(ishara) ambayo inatumka sana katika alama ya
kuwakilisha uislamu. Ishara(alama) hii
sio halisi katika uslamu. Ishara sio halisi katika uislamu.
Na ilikuwa alama ya washirikina iliyopitishwa wakati wa kuenea
kwa Uislamu, na matumizi yake leo hii wakati mwingine yanaleta utata katika
ulimwengu wa Kiislamu. Alama ya mwezi mpevu na nyota mara nyingi inasemwa ni
alama ya uislamu, lakini wanahistoria wanasema kwamba ilikuwa alama(ishara) ya
Dola ya Ottoman, si ya Kiislamu kwa ujumla.
Alama ya nyota na mwezi mpevu
ni misingi ya alama (ishara) zilizokuwa zinapatikana katika ulimwengu wa
kale pamoja na mifano ulioshuhudiwa
kutoka Bahari ya Mashariki, Uajemi na Asia ya Kati.
Alama(ishara) iliojitokeza katika matumizi maarufu katika
karne ya kumi na tisa(19) kama alama ya
kisasa ya taifa kwa Dola ya Ottoman wakati wa mageuzi ya kimagharibi ya
Tanzimat. Bendera ya Ottoman ya mwaka 1844 ilikuwa ya rangi nyeupe "ay-Yıldız"
(Kituruki kwa "mwezi mpevu na nyota") na nyuma ilikuwa na rangi
nyekundu.
inaendelea kuwa katika
matumizi kama bendera ya Jamhuri ya Uturuki pamoja na marekebisho madogo.
Mataifa
mengine zamani yalikuwasehemu ya Dola ya Ottoman na pia kutumia ishara au alama
ya nyota na mwezi mpevu, ikiwa ni pamoja na Libya (1951-1969 na baada ya 2011),
Tunisia (1956) na Algeria (1958). ishara hii ilitumika katika bendera za
mataifa mengine ya kitaifa ulioanzishwa wakati wa karne ya 20, ikiwa ni pamoja
na bendera ya Azerbaijan (1918), Pakistan (1947), Malaysia (1948), na
Mauritania (1959)..
KALE YA MSHARIKI ASIA
Nyota na Mwezi
mpevu ilionekana, kutumika ndani na nje ya Palestina ya kale. Imekuwa ikihusishwa na Wamoabi (karne ya14 au 13
mapema - karne ya 6 BC )., Kama ishara au alama kuonekana kwenye majina ya
mihuri ya Mmoabi (Moabite name seals).
Mwezi mpevu ulionekana pamoja na nyota au nyota ilikuwa alama ya kawaida ya Sumerian katika picha na kazi za sanaa.
Mwezi
mpevu umekuwa kawaida kuhusishwa na
mungu mwezi Sin (Nanna kwa Wasumeri) na nyota (mara nyingi kutambuliwa kama
Venus) na Ishtar (Inanna kwa Wasumeri). Na hii ilikuwa ikitumika mashariki ya
zamani katika bara Asia, hii miungu mwezi na nyota(nanna ,inanna ,sin au
ishtari) likuwa ni miungu ya kipagani karne za kale huko mashariki ya kati.
Mipango miji
Kipindi cha nyuma katika kupanga miji walitumia alama ya
nyota na mwezi ili kuweza pia kugundua sehemu zenye misikiti. Watu wa mipango
miji waliamua kutumia hizo alama na baada ya hapo baadhi ya misikiti ikaanza
kujengwa na kuekewa hizo alama za nyota na mwezi mpevu.Katika ramani mbalimbali
za kijiographia wanatuma alama ya nyota na mwezi na kwenye makanisa wanatumia
ishara ya msalaba.
Wanaotumia
Alama ya nyota na mwezi mpevu inatumika sehemu
mbalimbali katika dunia hii ya sasa na ilishatumika kipindi cha nyuma huko pia
·
Baadhi
bendera za nchi za kiislamu
Bendera ya Tunisia bendera ya pakistani
·
Mihuri
ya baadhi ya nchi za kiislamu
·
Nchi
zisizo za kiislamu
bendera ya singapore
·
Mashirika
ya kiislamu
·
Mashirika yasiyo ya kiislamu
JUMUISHO
Kuna baadhi ya watu au wasio amin Dini sahihi ya kiislamu
wakihusisha alama hizi kuwa ni katika
alama za uislamu . Na wakihusisha uislamu na kuabudu miungu ya kipagani ya
ishtari na sin(mungu nyota na mwezi) ambapo walikuwa wanaabudiwa na asumeri
mashariki ya Asia ya akale ambao hawakuwa waislamu. Na alama hii imetumika
sehemu mbalimbali Zaidi ya hizo nilizotaja
hapo awali
Katika kipindi cha Mtume Muhamadi(S.A.W) hakuwahi kutumia
alama hizi kama ishara au alama za kuonyesha uislamu
Allah (S.W) ndiye mjuzi.
Wabilahi Tawfiq
0 comments:
Post a Comment