Bi Harusi Kujipamba Katika Mipaka Ya Sheria
SWALI:
INSHAALLAH MUTAKUWA KATIKA HALI YA UZIMA NA MALIPO MEMA KWA ALLAH AMIN. SWALI LANGU VP BIHARUSI AJIPAMBE KAMA ILIVYOKUA KTK WAKE WA MTUME NA WATOTO WAKE JEE MAPAMBO YA SASA INAKUBALIKA KATIKA SHARIA KAMA VILE MAMEKAP NA KUPAKA PIKO NA UTOWAJI WA HALAWA {YAANI MALAIKA ZA MWILINI}. NA MA BLEACH NAOMBA MUNIJIBU MAPEMA SHUKRAN INSHAALLAH ALLAH ATAWALIPA. NAMI MUNIKUMBUKE KTK EMAIL YANGU IWE UEPESI KWANGU
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa ndugu yetu aliyeuliza swali. Uislamu ni mfumo kamili wa maisha, hivyo hakuna lolote isipokuwa umetupatia sisi jinsi ya kuliendea hilo . Mas-ala ya kujipamba si tofauti na mambo mengine. Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametuambia:
"Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote " (6: 38).
Uislamu umemruhusu na kumhimiza Muislamu ajipambe, avalie vizuri na kupendeza ili apate kustarehe na yale aliyoumbiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika mapambo, libasi (mavazi) na vyombo. Nayo mavazi katika Uislamu yana madhumuni mawili; kujisitiri utupu na kujipamba, na ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akawaneemesha wanaadamu wote kwa jumla kwa kuwatayarishia, kwa mipango Yake, mavazi na pambo, kama
Alivyoeleza katika Qur-aan:
"Enyi wanaadamu! Tumekuteremshieni nguo za kuficha tupu zenu, na nguo za pambo. Na nguo za ucha Mungu ndio bora. Hayo ni katika Ishara za Allaah mpate kukumbuka " (7: 26).
Tufahamu kuwa si bi harusi tu ambaye anafaa kujipamba katika mipaka ya sheria bali mwanamke ambaye ameolewa na mume ambaye ameoa wanafaa wote kujipamba kwa ajili ya mwenziwe. Mume anafaa ampambie mkewe na mke kumpambia mumewe.
Kuhusu pambo Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anatueleza:
"Sema: Ni nani aliyeharimisha pambo la Allaah Alilowatolea waja Wake, na vilivyo vizuri katika riziki. Sema hivyo ni kwa walioamini katika uhai wa duniani, na Siku ya Qiyaama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivi Tunazieleza Ishara kwa watu wanaojua " (7: 32).
Baada ya hayo itakuwa vyema tuangazie mapambo yanayokwenda sawa na sheria na yale ambayo yanakiuka mipaka ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala).
Ama kuhusu vipodozi (make-up) havina tatizo kuvitumia kwa kujipamba ukiwa kwa mumeo au nyumbani kwako na Maharimu zako, ikiwa havitakuwa na madhara. Tunavyofahamu vipodozi hivi vya sasa vinatengenezwa na kemikali. Ikiwa kutapatikana kuwa utumiaji una madhara na mwanaadamu basi havitakubaliwa na sheria kutumiwa. Hiyo ni kuwa msingi mkubwa wa sheria ni ile Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inayosema:
"Haifai kudhuru wala kulipana madhara" (Ibn Maajah na ad-Daraqutwniy, nayo ni Hasan).
Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametuonya pale Alipotuambia:
"Wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema. Hakika Allaah Huwapenda wafanyao wema" (2: 195).
Piko nayo ni aina ya urembo au pambo kama hinna hivyo hakutokuwa na utata wowote kuhusu matumizi yake. Hata hivyo zipo habari zinazotufikia kutoka kwa wake na dada zetu kuwa piko huwa ina athari kwa wengine wenye ugonjwa wa allergy (hasasiyah/ kuwa na mzio) na hivyo kumletea kuvimba kwa mwili na matatizo mengine ya kiafya. Pia zipo piko ambazo zinafanya ugozi kwenye ngozi hivyo kuzuia maji kufika kwenye ngozi wakati wa kutawadha au kuoga josho la janaba. Ikiwa piko kwako ina sifa ya kwanza au ya pili au zote mbili itakuwa haifai kwako kuitumia kwa misingi tuliyoeleza hapo juu.
Uislamu, kabla ya kushughulikia mapambo, kujitengeneza, ulisisitiza na kutilia mkazo mkubwa usafi na unadhifu kwa huo ndio chanzo cha kila pambo zuri na kila umbo jema. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"Hakika Allaah Aliyetukuka ni Mzuri na Hakubali ila zuri" (Muslim kutoka kwa Abu Hurayrah [Radhiya Allaahu 'anhu]).
Na amesema tena (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
"Jinadhifisheni kwani Uislamu ni Dini nadhifu" (Ibn Hibbaan).
"Jinadhifisheni kwani Uislamu ni Dini nadhifu" (Ibn Hibbaan).
Kwa ajili hii ndio Uislamu ukatuekea katika mambo ya Fitwrah (maumbile ya asli ya Uislam) ni kujisafisha. Katika kujiweka katika hali iliyo safi . Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituagizia:
" Mambo kumi ni katika Fitwrah (maumbile ya asli ya Kiislamu): 'Kupunguza masharubu, kufuga ndevu, kupiga mswaki, kupitisha maji puani (kusafisha), kukata kucha, kusafisha penyo za vidole, kung'ofoa (kunyoa) nywele za kwapa, kunyoa nywele za sehemu za siri, na kujisafisha kwa maji baada ya kujisaidia na msimuliaji akasema kasahau la kumi, lakini inaweza kuwa ni kusafisha mdomo (kusukutua)"
(Muslim na Abu Daawuud kutoka kwa mama wa waumini 'Aa'ishah [Radhiya Allaahu 'anha ]).
" Mambo kumi ni katika Fitwrah (maumbile ya asli ya Kiislamu): 'Kupunguza masharubu, kufuga ndevu, kupiga mswaki, kupitisha maji puani (kusafisha), kukata kucha, kusafisha penyo za vidole, kung'ofoa (kunyoa) nywele za kwapa, kunyoa nywele za sehemu za siri, na kujisafisha kwa maji baada ya kujisaidia na msimuliaji akasema kasahau la kumi, lakini inaweza kuwa ni kusafisha mdomo (kusukutua)"
(Muslim na Abu Daawuud kutoka kwa mama wa waumini 'Aa'ishah [Radhiya Allaahu 'anha ]).
Ukiyatizama mambo haya kumi utakuta yafuatayo ni kuweka unadhafa wa mwili, kwa mfano Kupunguza masharubu, kupiga mswaki, kupitisha maji puani (kusafisha), kukata kucha, kusafisha penyo za vidole, kung'ofoa (kunyoa) nywele za kwapa, kunyoa nywele za sehemu za siri, na kujisafisha kwa maji baada ya kujisaidia na lakini inaweza kuwa ni kusafisha mdomo (kusukutua). Hivyo, Muislamu amehimizwa kuweka usafi kwa kuosha viungo kadhaa, kutoa nywele ambazo ndio chanzo cha kuleta uchafu isipokuwa kunyoa ndevu (mwanaume) kumekatazwa kabisa.
Ama utoaji wa nywele ndogo ndogo ambazo baadhi ya watu huziita malaika!! hakuna tatizo lolote katika Dini ikiwa ni kwa sababu ya kujiremba au kujiweka katika hali ya usafi kama vile kunyoa nywele za kwapani na sehemu za siri. Ama katazo lililokuja ni kupunguza au kunyoa nyusi. Na amesema Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu):
"Allaah Amewalaani wenye kuchanja (tattoo), na wenye kuchanjwa (tattoo), na wenye kunyoa nyusi, na wenye kuchonga meno kwa urembo, na wenye kubadilisha umbile la Allaah. Akamuuliza yeye mwanamke kuhusu jambohilo . Akamjibu kwa kusema: "Kwa nini nisimlaani yule aliyelaaniwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na aliyelaaniwa katika Kitabu cha Allaah. Amesema Allaah Aliyetukuka:
'Na anachokupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho ' (59: 7)" (Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na an-Nasaa'iy).
Na katika Hadiyth nyingine tunaongezewa mapambo ambayo hayafai kufanywa na Muislamu. Na imepokewa kwa Asmaa' (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba mwanamke fulani alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
"Ewe Mtume wa Allaah! Binti yangu amepatwa na surua zikapuputika nywele zake, nami nimemuozesha; Je, niziunganishe?" Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu: "Allaah Amemlaani mwenye kuunganisha nywele zake (au nywele za mwengine kwa nywele nyengine) na mwenye kuungwa (au kuvaa nywele hizo )"
(Al-Bukhaariy, Muslim na an-Nasaaiy.
"Ewe Mtume wa Allaah! Binti yangu amepatwa na surua zikapuputika nywele zake, nami nimemuozesha; Je, niziunganishe?" Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu: "Allaah Amemlaani mwenye kuunganisha nywele zake (au nywele za mwengine kwa nywele nyengine) na mwenye kuungwa (au kuvaa nywele hizo )"
(Al-Bukhaariy, Muslim na an-Nasaaiy.
Na Hadiyth ya 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) imenukuliwa na al-Bukhaariy, Muslim na an-Nasaa'iy). Na katika riwaya nyengine:
"Mwenye kuunganisha nywele na mwenye kumtaka mwengine amfanyie kazi hiyo (mwenye kutamani kuzivaa nywele hizo za bandia)".
Na 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) amepokea mfano wake.
"Mwenye kuunganisha nywele na mwenye kumtaka mwengine amfanyie kazi hiyo (mwenye kutamani kuzivaa nywele hizo za bandia)".
Na 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) amepokea mfano wake.
Katika Hadiyth hizi na nyingine zilizo sahihi tunaelezewa kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza baadhi ya mapambo nayo ni, kutoa au kuchonga nyusi, kuunga nywele, kuchonga meno kwa urembo, kuchanja kwenye mwili kwa kujichora tattoo. Hivyo ni juu yetu kutahadhari na mapambo hayo kwani kuyafanya huwa tunaingia katika laana ya Allaah Aliyetukuka. Naye Allaah Aliyetukuka Anatufahamisha:
"Wao hawawaombi badala yake Yeye ila wanawake, wala hawamuombi ila Shetani aliye asi. Allaah Amemlaani. Naye Shetani alisema: Kwa yakini nitawachukua sehemu maalumu katika waja Wako. Na hakika nitawapoteza na nitawatia matamanio, na nitawaamrisha, basi watakata masikio ya wanyama, na nitawaamrisha, basi watabadili Aliyoumba Allaah. Na mwenye kumfanya Shetani kuwa ni mlinzi wake badala ya Allaah, basi huyo amekhasiri khasara ya dhahiri" (4: 117 – 119).
Ama kuhusu kutia bleach ili kubadili rangi ya mwili au kwa pambo hilo haliruhusiwi na Uislamu. Sababu ni kuwa huwa unabadilisha umbile alilokuumba nalo Allaah Aliyetukuka ambako kumekatazwa kama ilivyo Aayah iliyo juu (4: 117 – 119). Na pia bleach ni mchanganyiko wa makemikali ambayo yana madhara makubwa kwa mwili. Kwa sababu ya hiyo leo tunaona wanawake wenye kumea ndevu na kuwia vigumu kufanyiwa upasuaji kwa sababu ya ngozi ya juu kuathirika na kemikali na madhara mengine mengi. Kwa ajili hiyo ni juu yetu kuwakumbusha wenye kutumia wasijitie kwenye maangamivu na hivyo kuhasirika hapa duniani na Kesho Akhera.
Ingia katika kiungo kifuatacho pia upate maelezo zaidi kuhusu nywele:
Vifuatavyo ni vipodozi vya asli ambavyo vinafaa kutumia na vimeonekana kuwa vinaleta manufaa katika kuiboresha ngozi na nywele za mwanamke:
1. Hinna kwenye nywele.
2. Mchanganyiko wa mafuta ya lozi, nazi na zaytuni.
3. Majani ya mkunazi yaliyosagwa kwa ajili ya kusafishia uso.
4. Mchanganyiko wa Habba Sawdaa iliyosagwa na mafuta ya zaytuni upake usoni kisha ukae nayo katika jua kwa muda kidogo kisha uoshe.
Na Allaah Anajua zaidi.
0 comments:
Post a Comment