Saturday, 2 July 2016

NGUZO ZA IMANI

Unknown


Nguzo za Imani ni zile ambazo tunaamini katika uislamu. Imani ina maana kuamini kile usichokiona lakini una ushahidi wa kutosha juu ya kuwepo kwake, nah ii ndo maana ya Imani.
Kuna nguzo sita za Imani katika uislamu ambazo ni :
 1.Kumuamini Allah
 2.Kuamini malaika
 3.Kuamini mitume wa Allah
 4.Kuamini vitabu vya Allah
 5.Kuamini siku ya mwisho
 6.Kuamini Qadari (ya kheri au ya shari) kuwa inatoka kwa Allah).

1. Kumuamini Allah 

Hii ndo nguzo ya kwanza ya Imani katika uislamu. Kila muislamu anatakiwi awe na Imani juu ya kuwepo Allah(SW) ambaye ni mmoja na hajazaa wala hajazaliwa na hana mfano wake. Na sio kumuamini Allah peke yake lakini imeelezwa vizur katika kitabu kitukufu cha  Qur’an na Hadithi za Mtume Muhamadi (S.A.W). Pia inajumuisha majina 99 ya Allah(S.W)

2.Kuamini Malaika

Nguzo ya pili ya uislamu ni kuamini malaika wa Allah. Hawa ni malaika wa Allah. Na sio watoto wake kama baadhi wanavyodhani. Wameumbwa kutokana na mwanga na waliumbwa kabla ya kuumbwa binadamu kwa lengo la kumuabudu Allah(S.W).  Ili muislamu kuwa na imani thabiti anapaswa kuamini malaika wa Allah(S.W)

3. Kuamini mitume wa Allah(S.W)

Nguzo ya tatu ya uislamu ni kuamini mitume wa Allah. Wametajwa mitume  25 kwenye Qur’an tukufu . Na muislamu anatakiwa kuamini mitume wote walotajwa kwenye Qur’an kuwa ni mtume wa Allah. Na mtume Muhamadi(S.A.W) ndo mtume wa mwisho katika mitume wote na hakuna mtume baada yake na alitumwa kwa wote duniani kueneza dini ya uislamu na ndo dini ya ukwel.
  
4 Kuamini vitabu vya Allah(S.W)

Nguzo ya nne ya Imani ni kuamini vitabu vya Allah(S.W). Na hapa ni kuamini kwamba vitabu vyote vilivyotuma na Allah na ni ujumbe ulotoka Allah(S.W). Na kitabu kilichobakia ni Qur’an na ndo kitabu cha mwisho Allah alichokituma kwa wanadamu. Kuna vitabu vine vijulikanavyo kwa wanadamu navyo ni :

Taurati(Torah) kilitumwa na nabii Musa
Zabur(Psalms) kiltumwa na nabii Daudi(Dawud)
Injili kilitumwa na nabii Issa(Jesus)
Qur’an kilitumwa na Mtume Muhamadi(S.A.W)
Waislamu wanatakiwa kuamini vitabu vyote hvyo na sio Qur’an tu.

5. Kuamini siku ya mwisho

Nguzo ya tano ya uislamu ni kuamini kuwa kuna siku ya mwisho. Siku ya hukumu ya mema au maovu ,makubwa au madogo. Katika maisha  tunakaiwa kuamini kuwa kuna siku ya mwisho. Na Allah(S.W) ndo anajua ni siku hii siku ya mwisho itakuwa na hakuna kiumbe chochote kinachojua juu ya hilo. Tunatakiwa kuishi kila siku kama ndo sku yetu ya mwisho. Ishi katika duna kama mpita njia

6 . Kuamini Qadari (ya kheri au ya shari) kuwa inatoka kwa Allah).

Nguzo ya mwisho ya uislamu ni kuamini kuwa kuna Qadari. Kheri au shari zote znatoka kwa Allah. Inatakiwa kuamini kila kitu katika maisha yetu vilishaandikwa  . inatikiwa kuamini kwamba chochote Allah atakacho amua kutokea kitatokea kwasababu yeye ndo muumba wa kitu vilivyomo mbinguni na ardhini.

Hizi nguzo za Imani ndo misingi ya Imani kama muislamu. Nguzo za ndo msingi wetu wa Imani juu ya uislamu. Kuamini nguzo zote za Imani na kuzielewa ndio Imani thabiti.

Unknown / Author & Editor

12 comments:

Coprights @ 2016,