Friday, 8 July 2016

AINA TATU ZA NDOTO

Unknown
AINA TATU (3) ZA NDOTO

Asalam alyeikum:

Leo ningependa kuongelea aina tatu za ndoto:

Watu wengi wanapenda kujiuliza maswali mengi kuhusiana na ndoto. Unakuta mtu anakuambia nimeaota ndoto hii mara ile na wanauliza ndoto hii au ile ina maana gani ?
Unakuta mtu anakuaambia wakati naota nimeota mtu ananikimbiza na nilishindwa kukimbia Je hii ndoto nahusu nini.?
Na kuna wengine kati yetu tumewahi kuota angalau mara nne au mara tatu katika wiki nzima.
Na kuna wengine baadhi yetu wanaota kila siku usiku  mpaka wanashindwa kulala kutokana na ndoto mbaya wanazoota.

Kwa hiyo nataka kuongelea aina tatu tofauti za ndoto ambazo zimetajwa na Mtume Muhamad(S.A.W), Aina tatu za ndoto ni kama zifuatazo:


1.  Aina ya kwanza ni ile ndoto ambayo maono yake unayoona ni yale yatokayo kwa Allah(S.W) na Allah(S.W) anakuwa amekuonyesha hyo ndoto.

Unakuwa umeona kitu kilicho kizuri,unaona mwanga,unaona ndege wanapaa, au unaona mtu anakupa habari nzuri au unaona kitu ambacho huwez kukisahau(namaanisha huwezi kukisahau pale unapoamka siku inayofuata).

Kwanin ???

Kwasababu imekufanya uwe na furaha sana na imekufanya uweze kutabasamu,umeipenda na umecheka.

Sasa ndoto kama hizi zinatoka kwa Allah(S.W). Hizi ni ndoto zinazotoka kwa Allah(S.W)


2.  Aina ya pili ni ndoto ambazo huwa zinatokana na kufikiria sana kuhusu mambo mbalimbali katika  maisha yetu ya kila siku.

Mfano mtu anawaza vitu mpaka vinamfanya ashindwe kulala, mtu anawaza kuwa tajiri,awe na gari zuri ,nyumba nzuri, ameshika pesa au anabadlishana pesa. Hali hii ya kuwaza sana inaleta madhara kiakili na inasababisha mtu aweze kupata ndoto za aina kama hizo kutokana na msongo wa mawazo. Na inasababishwa na kufikiria sana kuhusu kitu au jambo.

3.  Aina ya tatu ni zile ndoto zinazotokana na shetani.

Na hizi ni zile ndoto ambazo zinakuwa zinatutisha. Ni zile ambazo unaamka katikati ya usku na ukajiuliza ni kweli bado niko hapa,Alhamdulilah.
Na unakuwa unahisi ile saa ambayo unakuwa umelala huwezi hata kunyanyua mkono,huwezi kusogea,huwezi kwenda kokote,unataka kuongea lakini huwezi kuongea.Hizi ni ndoto mbaya za usiku na zinatoka kwa shetani.

Ukiota ndoto kama hizi pale tu unapoamka unatakiwa kusema:

Ya Allah(S.W)[ewe Mwenyezi Mungu]  nilinde na shetani, Afu unatema mate kidogo sana(you blow) upande wa kushoto mara tatu, Na baada ya hapo unarudi kulala na usiwe na wasiwasi.

Kama ulikuwa umelalia upande wa kushoto unaeza lala kwa upande wa kulia. Na ulikuwa umelalia upande wa kulia unaeza lala kw upande wa kushoto.

Na kutokana na ndoto hizi hutakiwi kuwaza wala kuzifikiria kuhusu ulichoota na usimwambe mtu maana ni ndoto zitokanazo na shetani.
Maana shetani anachotaka kufanya ni kwamba uogope uwe na wasiwasi na ushindwe kujihusisha na masuala ya dini yako na ushindwe kujihusisha na kufanya ibada na ukae uanze kufikiri ndoto mbaya uliyoota.

Lakini ndoto ambayo utaota katika aina ya kwanza ya ndoto zitokazo kwa Allah(S.W) unaruhusiwa kuwaambia wale watu uwapendao na walio karibu na wewe. Ni sunnah kuwaambia wale uwapendao.

Mfano umeota ndoto nzuri usiku ukiamka kesho yake unaeza ukamwambia mke wako kama unampenda ,ukawaambia wazazi wako,ukawaambia familia yako,ukawaambia watoto wako.
Ila usiwaambie watu ambao hawakupendi, kama unakumbuka historia ya Yakubu(A.S) ambapo Yusufu aliona kwenye ndoto wakati amelala sayari kumi na moja(11) zinamsujudia. Na Yakubu(A.S) alimwambi usiwaambe kaka zako.

Kwanini ?

Kwasababu kaka zake walikuwa na utashi,walikuwa wanamchukia.
Kwa hiyo tusiwe tunawambia ndoto zetu nzuri watu wanaotuchukia, tuwaambie wale tu wanaotupenda.

Na kwa ndoto mbaya zitokanazo na shetani tusimwambie mtu yoyote yule.

Tumuombe Allah(S.W) atuongoze katika njia iliyonyooka na sio njia ya wale aliowakasirikia.



                                   


Unknown / Author & Editor

0 comments:

Post a Comment

Coprights @ 2016,