Tuesday, 16 August 2016

USIKU WA HARUSI (NDOA)

Unknown

Mlango 1: Usiku Wa Harusi (Ndoa)

A’mali Za Usiku Wa Harusi




 Imesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w) kwamba:Milango ya Peponi kwa ajili ya rehema itafunguliwa katika hali nne: Wakati inaponyesha mvua; wakati mtoto anapoangalia kwa huruma usoni kwa mzazi wake; pale mlango wa Ka’ba unapokuwa wazi, na wakati wa (kutokea) harusi.
Kama inavyoonyeshwa na hadithi hiyo hapo juu, dhana ya harusi katika Uislam ni tukufu mno na yenye kuthaminiwa, kiasi kwamba milango ya rehema ya Mwenyezi Mungu inafunguliwa katika tukio hili.
Naam, hili halishangazi pale mtu anapochukulia kwamba ndoa inahifadhi sehemu kubwa ya imani ya mtu na kuilinda na uovu wa Shetani, kama ilivyosimuliwa kutoka kwa Mtume (s.a.w):

 “Hakuna kijana yeyote atakayefunga ndoa katika ujana wake, isipokuwa kwamba shetani wake anapiga makelele akisema: ‘Ole wake, ole wake, amezikinga sehemu mbili ya tatu ya imani yake kutokana na mimi;’ 

kwa hiyo mwanadamu lazima awe na taqwa (mwenye kumcha Mungu) kwa Mwenyezi Mungu ili kulinda sehemu moja ya tatu ya imani yake iliyobakia.
Ni muhimu kwa hiyo, kwamba wawili hao, pale wanapoingia kwenye hatua hii, wachukue hadhari ya hali ya juu kulinda usafi wa muungano huu mtukufu na wala wasiutie doa tangu mwanzoni mwake kwa kuruhusu lile tukio la sherehe ya harusi kuwa ni chanzo cha madhambi na israaf.
Hususan ule usiku wa harusi ndio usiku wa kwanza ambao mwanaume na mwanamke wanakuja pamoja kama mume na mke, na imekokotezwa sana kwamba wanaunda muungano huo kwa nia ya kupata ukaribu na radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu na kufanya zile A’amali zilizopendekezwa kwa ajili ya usiku huo.
Wakati huu ni muhimu kuangalia ni hali gani yule ‘Bibi wa wanawake wote wa ulimwengu,’ Hadhrat Fatimah (a.s.) aliyokuwa nayo ule usiku wa harusi yake, na ni vipi alianza maisha yake na mume wake, Imam Ali (a.s.): Katika ule usiku wa harusi Imam Ali (a.s.) alimuona Hadhrat Fatimah (a.s.) alikuwa amefadhaika na akitokwa na machozi, na akamuuliza kwa nini alikuwa kwenye hali ile.
Yeye alijibu akasema: “Nilifikiria kuhusu hali yangu na vitendo na nikakumbuka mwisho wa uhai na kaburi langu; kwamba leo nimeondoka nyumbani kwa baba yangu kuja nyumbani kwako, na siku nyingine nitaondoka hapa kwenda kaburini na Siku ya Kiyama.
Kwa hiyo, namuapia Mungu juu yako; njoo tusimame kwa ajili ya swala ili kwamba tuweze kumuabudu Mwenyezi Mungu pamoja katika usiku huu.

A’amali Zifuatazo Zinapendekezwa Kwa Ajili Ya Usiku Huu

A’amali Zifuatazo Zinapendekezwa Kwa Ajili Ya Usiku Huu

1.  Jaribu kuwa katika Udhuu kwa kiasi kirefu kinachowezekana cha usiku huo, na                  hususan wakati wa A’amal zifuatazo hapa chini.
2.   Anza kwa kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu halafu useme “Allahu Akbar,”                    ikifuatiwa na Swala ya Mtume – Allahumma swali ‘alaa Muhammadin wa aali                         Muhammad).
3.  Swali rakaa mbili, kwa nia ya ‘Mustahab Qurbatan ilallah’ – kujisogeza karibu na                 Allah (s.w.t.). (Swala inayopendekezwa kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi                    Mungu) ikufuatiwa na Swala
       ya Mtume.
4.  Soma Dua ifuatayo, ikifuatiwa na Swala ya Mtume. Kwanza bwana harusi aanze                  kuisoma, baada yake ambapo bibi harusi atapaswa kusema: Ilahi Amin (Mwenyezi            Mungu aitakabalie Dua hii).
Allahumma rzuqniy ilfahaa wa wudhahaa wa ridhwaahaa wa radhwiniy bihaa thumma j’ma’u bayinanaa bi-ahsani j’timaa’in wa asarri itilaafin fainnaka tuhibbul-halaala wa takrahul-haraam.”
Ewe Allah! Nijaalie na upendo wake, mapenzi na kunikubali kwake mimi; na nifanye mimi niridhike naye, na tuweke pamoja katika namna bora ya muungano na katika muafaka kamilifu, hakika Wewe unapenda mambo ya halali na unachukia yale ya haram.”

5.  Hata kama wawili hao hawadhamirii kushika mimba katika usiku huo wa harusi,               inapendekezwa kwamba Dua zifuatazo zisomwe kwa ajili ya watoto wazuri (wakati          wowote itakapotunga mimba):

a. Bwana harusi anapaswa aweke kiganja cha mkono wake wa kulia kwenye paji la uso      la bibi harusi kwa kuelekea Qibla na asome:
Allahumma bi-amaanatika akhadhtuhaa wa bikalimaatika stahlaltuhaa fain qadhwayta liy minhaa waladaan faaj’alhu mubaarakaan taqiyyan minshiy’ati aali Muhammad wa laa taj’al lil-shaytwaani fiyhi shirkaan wa laa naswiybaan.
Ewe Allah! Nimemchukua (binti) huyu kama amana Yako na nimemfanya halali juu yangu mwenyewe kwa maneno Yako. Kwa hiyo, kama umenikadiria mtoto kutokana naye, basi mfanye mbarikiwa na mchamungu kutoka miongoni mwa wafusi wa familia ya Muhammad; na usimfanye Shetani kuwa na sehemu yoyote ndani yake.”

b. Dua ifuatayo pia inapaswa kusomwa:
“Allahumma bi-kalimaatika stahlaltuhaa wa bi-amaanatika akhadhtuhaa. Allahumma-j’alhaa waluwdaan waduwdaan laa tafraku taakulu mimmaa raaha wa laa tas-alu ‘ammaa saraha.”
Ewe Allah! Nimemfanya awe halali juu yangu kwa maneno Yako, na nimemchukua katika amana Yako. Ewe Allah! Mjaalie awe mwenye kuzaa na mwenye upendo.”

6.  Bwana harusi aioshe miguu ya bibi harusi na anyunyize maji hayo katika pembe               zote nne za chumba na nyumba. Mwenyezi Mungu Mtukufu ataondoa aina 70,000 za       umasikini, aina 70,000 za neema zitaingia ndani ya nyumba hiyo na neema 70,000           zitakuja juu ya bibi na bwana harusi. Bibi harusi atakuwa salama kutokana na                     wendawazimu, vidonda vya tumbo na ukoma.

Baadhi Ya Mambo Kwa Ajili Ya Bibi Na Bwana Harusi

1. Sio lazima kwamba kujamiiana kwa kutimiza ndoa kufanyike katika ule usiku wa              harusi; bali unaweza kuchukua siku chache au hata majuma machache.
2. Uchovu, wasiwasi na fadhaa vinaweza kufanya hilo liwe gumu zaidi; hivyo ni muhimu     kwamba mume na mke wachukue muda wa kutosha kuweza kuwa wametulizana na       kuzoeana na kwenda kwa mwendo wao wenyewe.
3. Mafuta ya kulainishia yanaweza yakahitajika kwa siku zile chache za mwanzo au                majuma ili kufanya kule kujamiiana kuwa rahisi zaidi na kwenye starehe zaidi.
4. Kumaliza mapema au kusikotarajiwa kunaweza kuwa ni tatizo kwa mara chache za          mwanzoni; hata hivyo, hili linapaswa kutatuliwa baada ya kupita muda na                            kupatikana uzoefu.
5. Kizinda (cha bikra) kinaweza kivuje au kisivuje damu. Unyegereshano, upole  na               kuingiliana tena mara tu baada ya hapo kunaweza kupunguza maumivu ya                          uchanikaji wa hicho kizinda.
6. Baada ya kujamiiana (wakati wowote itakapokuwa), bibi harusi asije akatumia                 maziwa, siki, giligilani, tuhafa chungu au tikitimaji kwa kiasi cha juma moja, kwani           vinasababisha tumbo la uzazi kukauka na kuwa la baridi na gumba. Kula siki wakati       huu vilevile kunatokezea kwa mwanamke kutokuwa msafi (tohara) kutokana na               damu ya hedhi, giligilani (na tikitimaji) kunasababisha matatizo ya wakati wa                     uchungu na tuhafa linasababisha kusimamisha ukawaida wa hedhi, na yote haya             yanaishia kwenye kuleta maradhi.
7. Watu wanaweza wakatoa maoni fulani juu ya siku chache zinazofuatia. Ni muhimu          sana kufanya hilo lisikuathiri wewe, na usivutike kwenye mazungumzo yao.
8. Usizungumze kuhusu mambo yako ya ndani kwa watu wa nje, chunga heshima kwa        mwenza wako na kwenye uhusiano wenu.


Saturday, 6 August 2016

JINSI YA KUMFURAHISHA MUME

Unknown

Mapokezi mazuri

a)   Baada ya kurejea kutoka kazini, skuli, safarini, au popote  pale palipowatenganisha, anza kwa maamkizi mazuri.
b)   Mpokee kwa uso mchangamfu
c)     Jipambe na ujitie manukato (Perfume)
d)    Anza na habari nzuri na chelewesha habari yoyote  mbaya mpaka atapokwisha pumzika
e)     Mpokee kwa maneno ya mapenzi na hamu/shauku
f)     Fanya jitihada kubwa katika mapishi mazuri na  kitayarishe kwa wakati.

 Ipambe na ilainishe sauti


a)   Ni kwa ajili ya mumeo peke yake, isitumike mbele ya wanaume wasio mahram (wanaume wanaoweza     kukuoa iwapo utakuwa huna mume)
              
Harufu nzuri na kujipamba mwili

a)      Ushughulikie vyema mwili wako na afya yako.
b)      Vaa nguo za kuvutia na jitie manukato.
c)     Koga mara kwa mara, na baada ya siku za hedhi, safisha  madoa madoa yote ya damu na ondosha  harufu mbaya.
d)    Jiepushe kuonekana na mumeo ukiwa na nguo chafu au ukiwa ovyo.
e)    Jiepushe na mapambo yaliyokatazwa, mfano wa tattoo.(kuchorwa mwili kwa kitu cha moto kwa ajili ya pambo.)
f)      Tumia aina ya manukano, rangi, na nguo ambazo mumeo anazipenda.
g)    Badilisha mtindo wa nywele, manukato n.k. mara kwa mara.
h)    Hata hivyo usifanye israfu katika vitu hivi, na bila shaka fanya hivyo mbele ya mahram zako na wanawake wenzako tu.

Jimai (Tendo la ndoa)

a)      Harakisha kufanya jimai pale mumeo anapokuwa na hamu ya tendo hilo.
b)   Weka mwili wako safi na wenye kunukia kadri iwezekanavyo pamoja na kujisafisha maji maji yanayotoka wakati wa jimai.
c)     Semeshaneni maneno ya mapenzi na mumeo.
d)    Mwachie mumeo atosheleze kabisa hamu yake.
e)    Chagua wakati muwafaka na muda mzuri wa kumchangamsha mumeo, na kumtia hamu ya kufanya jimai, mfano baada ya kurudi safari, mwisho wa wiki, n.k.

 Kutosheka na kile ulichojaaliwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

a)   Usiwe mnyonge kwa kuwa mumeo ni maskini au na aina ya kazi  anayofanya.
b)    Uwaangalie masikini, wagonjwa, na vilema na kumkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa yote yale uliyopewa.
c)   Ni lazima ukumbuke kuwa utajiri wa kweli upo katika Iman na uchaji Allaah.
       
 Kutoshughulishwa na mambo ya kidunia          

a)    Usiichukulie dunia hii kuwa ya matumaini na kushughulishwa nayo.
b)    Usimdai mumeo vitu vingi visivyo na ulazima.
c)    Kutosheka na kuishi maisha ya kawaida hakuna maana ya kutofurahia/kutotumia kilicho kizuri na kilichoruhusiwa (halali), bali kunamaanisha mtu kuangalia akhera yake na kutumia kile ambacho Allaah Amempa kwa ajili ya kupata Pepo (Jannah).
d)    Muhimize mumeo kupunguza matumizi na kubakisha fedha kwa ajili ya kutoa sadaka na kuwalisha masikini na wasiojiweza

Shukurani

a)    Kutokana na hadithi ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wengi wa watu wa motoni ni wanawake kwa sababu hawana shukurani na kutoridhia wema wanaofanyiwa.
b)   Matokeo ya kuwa na shukurani ni kuwa mumeo atakupenda zaidi na atafanya awezalo kukufurahisha kwa njia nyingi.
c)    Matokeo ya kutokuwa na shukurani ni kuwa mumeo atavunjika moyo na ataanza kujiuliza: Kwa nini nilazimike kumfanyia wema hali ya kuwa hana shukurani?
Kujitolea na Twaa

a)    Hususan nyakati za maharibiko/matatizo makubwa katika mwili wa mumeo au katika kazi yake, mfano  ajali au kufilisika.
b)   Kumpa msaada kwa kufanya kazi,  msaada wa fedha, na vitu vyengine iwapo utahitajika.

Kumtii

a)    Kumtii katika yote anayokuamrisha, isipokuwa katika yale  yaliyoharamishwa.
b)   Katika Uislam, mume ndie kiongozi wa familia, na mke ni msaidizi na mshauri wake.

Kumliwaza anapokasirika

 a)   Kwanza kabisa, jaribu kujiepusha na kile ambacho una uhakika kuwa kitamkasirisha.
b)   Bali iwapo imetokezea kuwa huwezi, basi jaribu kuepusha ugomvi kwa njia zifuatazo:
      1.    Iwapo wewe ndiye uliyekosea, basi mtake radhi (muombe msamaha)
      2.     Iwapo yeye ndiye aliyekosea basi:
-    Endelea kunyamaza badala ya kubishana au
    Samehe haki yako au
-     Subiri hadi zitakapokwisha hasira zake na mlijadili suala hilo kwa    amani
3.    Iwapo amekasirishwa na mambo nje ya nyumba basi:
           -    Endelea kunyamaza kimya hadi hasira zake zitapokwisha
                     -       Mpe udhuru (wa hasira zake), mfano kuchoka, matatizo kazini, kuna mtu amemuudhi.
-   Usimuulize masuala mengi na kushikilia kujua nini kimetokezea, mfano (kumwambia) (1) Ni lazima unieleze nini kimetokezea.  (2) Ni lazima nijue nini kimekukasirisha namna hiyo. (3) Unanificha kitu, na mimi nina haki ya kujua.

Muongozo (na majukumu) anapokuwa hayupo

a)      Jilinde na mahusiano yoyote yaliyokatazwa.
b)    Zidhibiti siri za familia, hususan jimai (tendo la ndoa) na  mambo ambayo mumeo hapendi watu wengine wayajue.
c)      Ishughulikie nyumba na watoto.
d)      Ishughulikie mali yake na vitu vyake.
e)      Usitoke nje ya nyumba yako bila ya ruhusa yake na bila ya hijaab iliyo kamili.
f)       Usikaribishe watu ambao mumeo hapendi kuja kwao.
g)      Usimruhusu mwanamme yeyote asie Mahram wako kuwa nawe faragha pahala popote.
h)      Kuwa mwema kwa wazazi wake na jamaa zake akiwa hayupo.

Kuonyesha heshima kwa familia yake na rafiki zake

a)   Ni lazima uwakaribishe wageni wake na ujaribu kuwafurahisha, hususan wazazi wake.
b)   Ni lazima uepuke matatizo kati yako na jamaa zake kwa kadri iwezekanavyo.
c)   Ni lazima uepuke kumuweka pahala ambapo inambidi  achague kati ya mama yake na mkewe.
d)  Onyesha urafiki (makaribisho mazuri) kwa wageni wake kwa kuwatayarishia pahala pazuri pa kuketi, chakula kizuri, kuwakaribisha vizuri wake zao, n.k.
e)   Muhimize kuwatembelea jamaa zake na uwaalike nyumbani kwako.
f)   Wapigie simu wazazi na dada zake, watumie barua, na wanunulie zawadi, wasaidie wakati wanapoharibikiwa, n.k.

Wivu wenye kukubalika

a)     Wivu ni aina ya mapenzi ya mke kwa mumewe bali ni lazima ubakie katika mipaka ya Uislam, mfano  kutowatukana na kuwasengenya wengine, kuwavunjia heshima zao, n.k.
b)      Usifuate au kuanzisha tuhuma zisizo na msingi

Subira na kumpa moyo

a)      Kuwa na subira mnapokabiliwa na umasikini na hali ngumu (kimaisha  na kifamilia).
b)    Wakati mnapokabiliwa na majanga na maharibiko ambayo yanaweza kutokea kwako, kwa mumeo, kwa watoto wako, jamaa au mali, mfano magonjwa, ajali, kifo, n.k.
c)    Wakati mnapokabiliwa na matatizo katika Da’wah (kufungwa jela, kukamatwa, n.k.), kuwa na subira na mhimize katika kubaki katika njia ya Allaah na kumkumbusha kuhusu Pepo.
d)    Anapokufanyia uovu, mlipe uovu wake kwa kumfanyia wema.

Msaidie katika kumtii Allaah, Da'awah (Ulinganiaji) na Jihaad

a)      Shirikiana na mumeo na mkumbushe ibada mbali mbali za   faradhi na za Sunnah.
b)     Muhimize kusali usiku.
c)    Sikiliza na soma Qur-aan peke yako na ukiwa pamoja na mumeo.
d)    Mkumbuke (mtaje) Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) sana, hasa hasa baada ya Alfajiri na kabla ya Magharibi.
e)   Pangeni pamoja shughuli za Da’wah kwa wanawake na  watoto.
f)     Jifunze hukumu za Kiislam na adabu za Kiislam kwa wanawake.
g)    Msaidie mumeo katika shughuli zake kwa kumhimiza, kumpa ushauri mwema, kumliwaza machungu yake, n.k.
h)      Samehe baadhi ya haki zako na samehe sehemu ya muda wako wa kuwa pamoja na mumeo kwa ajili ya Da’wah.
i)      Mhimize kwenda Jihad anapohitajika na mkumbushe kuwa wewe na watoto mtakuwa katika hifadhi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). 

 Utunzaji mzuri wa Nyumba

a)   Iweke nyumba safi, weka mapambo na iweke katika mpangilio mzuri.
b)    Badilisha mpangilio wa nyumba mara kwa mara ili kuzuia kupoteza hamu nayo na kuchoshwa nayo.
c)    Tayarisha chakula kizuri na chenye afya.
d)   Jifunze ujuzi wowote wa muhimu kuhusu uangalizi wa nyumba, mfano kushona, n.k.
e)   Jifunze namna ya kuwalea vyema watoto na kwa njia ya Kiislam.
Kuhifadhi/Kutunza fedha na familia

a)   Usitumie fedha zake, hata kwa sadaka bila ya ruhusa yake labda uwe na uhakika kuwa atakubaliana na matumizi hayo.
b)   Ilinde nyumba yake, gari, n.k. anapokuwa hayupo.
c)    Waweke watoto katika hali nzuri, nguo safi, n.k. Zingatia lishe yao, afya, elimu, tabia, n.k wafunze Uislam na wahadithie visa vya Mitume ('Alayhimus Salaam) na Maswahaba (Radhiya Allaahu 'anhum).
  

Tuesday, 2 August 2016

BI HARUSI KUJIPAMBA

Unknown

Bi Harusi Kujipamba Katika Mipaka Ya Sheria

   
SWALI:
INSHAALLAH MUTAKUWA KATIKA HALI YA UZIMA NA MALIPO MEMA KWA ALLAH AMIN. SWALI LANGU VP BIHARUSI AJIPAMBE KAMA ILIVYOKUA KTK WAKE WA MTUME NA WATOTO WAKE JEE MAPAMBO YA SASA INAKUBALIKA KATIKA SHARIA KAMA VILE MAMEKAP NA KUPAKA PIKO NA UTOWAJI WA HALAWA {YAANI MALAIKA ZA MWILINI}. NA MA BLEACH NAOMBA MUNIJIBU MAPEMA SHUKRAN INSHAALLAH ALLAH ATAWALIPA. NAMI MUNIKUMBUKE KTK EMAIL YANGU IWE UEPESI KWANGU 



JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa ndugu yetu aliyeuliza swali. Uislamu ni mfumo kamili wa maisha, hivyo hakuna lolote isipokuwa umetupatia sisi jinsi ya kuliendea hilo. Mas-ala ya kujipamba si tofauti na mambo mengine. Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametuambia:
"Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote " (6: 38).

Uislamu umemruhusu na kumhimiza Muislamu ajipambe, avalie vizuri na kupendeza ili apate kustarehe na yale aliyoumbiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika mapambo, libasi (mavazi) na vyombo. Nayo mavazi katika Uislamu yana madhumuni mawili; kujisitiri utupu na kujipamba, na ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akawaneemesha wanaadamu wote kwa jumla kwa kuwatayarishia, kwa mipango Yake, mavazi na pambo, kama
Alivyoeleza katika Qur-aan:
"Enyi wanaadamu! Tumekuteremshieni nguo za kuficha tupu zenu, na nguo za pambo. Na nguo za ucha Mungu ndio bora. Hayo ni katika Ishara za Allaah mpate kukumbuka " (7: 26).
Tufahamu kuwa si bi harusi tu ambaye anafaa kujipamba katika mipaka ya sheria bali mwanamke ambaye ameolewa na mume ambaye ameoa wanafaa wote kujipamba kwa ajili ya mwenziwe. Mume anafaa ampambie mkewe na mke kumpambia mumewe.
Kuhusu pambo Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anatueleza:
"Sema: Ni nani aliyeharimisha pambo la Allaah Alilowatolea waja Wake, na vilivyo vizuri katika riziki. Sema hivyo ni kwa walioamini katika uhai wa duniani, na Siku ya Qiyaama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivi Tunazieleza Ishara kwa watu wanaojua " (7: 32).
Baada ya hayo itakuwa vyema tuangazie mapambo yanayokwenda sawa na sheria na yale ambayo yanakiuka mipaka ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala).
Ama kuhusu vipodozi (make-up) havina tatizo kuvitumia kwa kujipamba ukiwa kwa mumeo au nyumbani kwako na Maharimu zako, ikiwa havitakuwa na madhara. Tunavyofahamu vipodozi hivi vya sasa vinatengenezwa na kemikali. Ikiwa kutapatikana kuwa utumiaji una madhara na mwanaadamu basi havitakubaliwa na sheria kutumiwa. Hiyo ni kuwa msingi mkubwa wa sheria ni ile Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inayosema:
"Haifai kudhuru wala kulipana madhara" (Ibn Maajah na ad-Daraqutwniy, nayo ni Hasan).
Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametuonya pale Alipotuambia:
"Wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema. Hakika Allaah Huwapenda wafanyao wema" (2: 195).

Piko nayo ni aina ya urembo au pambo kama hinna hivyo hakutokuwa na utata wowote kuhusu matumizi yake. Hata hivyo zipo habari zinazotufikia kutoka kwa wake na dada zetu kuwa piko huwa ina athari kwa wengine wenye ugonjwa wa allergy (hasasiyah/ kuwa na mzio) na hivyo kumletea kuvimba kwa mwili na matatizo mengine ya kiafya. Pia zipo piko ambazo zinafanya ugozi kwenye ngozi hivyo kuzuia maji kufika kwenye ngozi wakati wa kutawadha au kuoga josho la janaba. Ikiwa piko kwako ina sifa ya kwanza au ya pili au zote mbili itakuwa haifai kwako kuitumia kwa misingi tuliyoeleza hapo juu.
Uislamu, kabla ya kushughulikia mapambo, kujitengeneza, ulisisitiza na kutilia mkazo mkubwa usafi na unadhifu kwa huo ndio chanzo cha kila pambo zuri na kila umbo jema. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"Hakika Allaah Aliyetukuka ni Mzuri na Hakubali ila zuri" (Muslim kutoka kwa Abu Hurayrah [Radhiya Allaahu 'anhu]).
Na amesema tena (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 "Jinadhifisheni kwani Uislamu ni Dini nadhifu" (Ibn Hibbaan).
Kwa ajili hii ndio Uislamu ukatuekea katika mambo ya Fitwrah (maumbile ya asli ya Uislam) ni kujisafisha. Katika kujiweka katika hali iliyo safi. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituagizia:

 " Mambo kumi ni katika Fitwrah (maumbile ya asli ya Kiislamu): 'Kupunguza masharubu, kufuga ndevu, kupiga mswaki, kupitisha maji puani (kusafisha), kukata kucha, kusafisha penyo za vidole, kung'ofoa (kunyoa) nywele za kwapa, kunyoa nywele za sehemu za siri, na kujisafisha kwa maji baada ya kujisaidia na msimuliaji akasema kasahau la kumi, lakini inaweza kuwa ni kusafisha mdomo (kusukutua)

(Muslim na Abu Daawuud kutoka kwa mama wa waumini 'Aa'ishah [Radhiya Allaahu 'anha ]).
Ukiyatizama mambo haya kumi utakuta yafuatayo ni kuweka unadhafa wa mwili, kwa mfano Kupunguza masharubu, kupiga mswaki, kupitisha maji puani (kusafisha), kukata kucha, kusafisha penyo za vidole, kung'ofoa (kunyoa) nywele za kwapa, kunyoa nywele za sehemu za siri, na kujisafisha kwa maji baada ya kujisaidia na lakini inaweza kuwa ni kusafisha mdomo (kusukutua). Hivyo, Muislamu amehimizwa kuweka usafi kwa kuosha viungo kadhaa, kutoa nywele ambazo ndio chanzo cha kuleta uchafu isipokuwa kunyoa ndevu (mwanaume) kumekatazwa kabisa.
Ama utoaji wa nywele ndogo ndogo ambazo baadhi ya watu huziita malaika!! hakuna tatizo lolote katika Dini ikiwa ni kwa sababu ya kujiremba au kujiweka katika hali ya usafi kama vile kunyoa nywele za kwapani na sehemu za siri. Ama katazo lililokuja ni kupunguza au kunyoa nyusi. Na amesema Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu):

"Allaah Amewalaani wenye kuchanja (tattoo), na wenye kuchanjwa (tattoo), na wenye kunyoa nyusi, na wenye kuchonga meno kwa urembo, na wenye kubadilisha umbile la Allaah. Akamuuliza yeye mwanamke kuhusu jambohilo. Akamjibu kwa kusema: "Kwa nini nisimlaani yule aliyelaaniwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na aliyelaaniwa katika Kitabu cha Allaah. Amesema Allaah Aliyetukuka:
'Na anachokupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho ' (59: 7)" (Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na an-Nasaa'iy).
Na katika Hadiyth nyingine tunaongezewa mapambo ambayo hayafai kufanywa na Muislamu. Na imepokewa kwa Asmaa' (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba mwanamke fulani alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 "Ewe Mtume wa Allaah! Binti yangu amepatwa na surua zikapuputika nywele zake, nami nimemuozesha; Je, niziunganishe?" Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu: "Allaah Amemlaani mwenye kuunganisha nywele zake (au nywele za mwengine kwa nywele nyengine) na mwenye kuungwa (au kuvaa nywele hizo )" 

(Al-Bukhaariy, Muslim na an-Nasaaiy.
Na Hadiyth ya 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) imenukuliwa na al-Bukhaariy, Muslim na an-Nasaa'iy). Na katika riwaya nyengine:

 "Mwenye kuunganisha nywele na mwenye kumtaka mwengine amfanyie kazi hiyo (mwenye kutamani kuzivaa nywele hizo za bandia)". 

Na 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) amepokea mfano wake.
Katika Hadiyth hizi na nyingine zilizo sahihi tunaelezewa kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza baadhi ya mapambo nayo ni, kutoa au kuchonga nyusi, kuunga nywele, kuchonga meno kwa urembo, kuchanja kwenye mwili kwa kujichora tattoo. Hivyo ni juu yetu kutahadhari na mapambo hayo kwani kuyafanya huwa tunaingia katika laana ya Allaah Aliyetukuka. Naye Allaah Aliyetukuka Anatufahamisha:
"Wao hawawaombi badala yake Yeye ila wanawake, wala hawamuombi ila Shetani aliye asi. Allaah Amemlaani. Naye Shetani alisema: Kwa yakini nitawachukua sehemu maalumu katika waja Wako. Na hakika nitawapoteza na nitawatia matamanio, na nitawaamrisha, basi watakata masikio ya wanyama, na nitawaamrisha, basi watabadili Aliyoumba Allaah. Na mwenye kumfanya Shetani kuwa ni mlinzi wake badala ya Allaah, basi huyo amekhasiri khasara ya dhahiri" (4: 117 – 119).
Ama kuhusu kutia bleach ili kubadili rangi ya mwili au kwa pambo hilo haliruhusiwi na Uislamu. Sababu ni kuwa huwa unabadilisha umbile alilokuumba nalo Allaah Aliyetukuka ambako kumekatazwa kama ilivyo Aayah iliyo juu (4: 117 – 119). Na pia bleach ni mchanganyiko wa makemikali ambayo yana madhara makubwa kwa mwili. Kwa sababu ya hiyo leo tunaona wanawake wenye kumea ndevu na kuwia vigumu kufanyiwa upasuaji kwa sababu ya ngozi ya juu kuathirika na kemikali na madhara mengine mengi. Kwa ajili hiyo ni juu yetu kuwakumbusha wenye kutumia wasijitie kwenye maangamivu na hivyo kuhasirika hapa duniani na Kesho Akhera.
Ingia katika kiungo kifuatacho pia upate maelezo zaidi kuhusu nywele: 
Vifuatavyo ni vipodozi vya asli ambavyo vinafaa kutumia na vimeonekana kuwa vinaleta manufaa katika kuiboresha ngozi na nywele za mwanamke:
1.     Hinna kwenye nywele.
2.     Mchanganyiko wa mafuta ya lozi, nazi na zaytuni.
3.     Majani ya mkunazi yaliyosagwa kwa ajili ya kusafishia uso.
4.     Mchanganyiko wa Habba Sawdaa iliyosagwa na mafuta ya zaytuni upake usoni kisha ukae nayo katika jua kwa muda kidogo kisha uoshe.            
Na Allaah Anajua zaidi.

Coprights @ 2016,