JINSI YA KUONGEZA KUMBUKUMBU (MEMORY)
Hii ni ya muhimu sana ndugu zangu
waislamu kama unataka kusoma au kupata elimu juu ya vitu mbalimbali. Kama ungependa
kujua ,kama ungependa kuongeza ujuzi au elimu yako unatikiwa uache kufanya dhambi
.
ALLAH (S.W) anasema “ Mfahamu ALLAH(S.W) na ALLAH(S.W) atakufundisha
na ALLAH(S.W) atahakikisha unajua na ujuzi wako utaongezeka”
Unajua Imamu Shafii(R.A) jina
lake lilikuwa ni Muhamad Ibn Idrees Ash Shafii, aliwah kulalamika kwa mmoja
wawafuasi wake anejulikana kwa jina la Waki Ibn Al Jarrah(R.A) “ Na anasema nimewahi kulalamika kwa Wakii Ibn
Jarrah kuhusu kumbukumbu yangu” na imamu Shafi alikuwa na kumbukumbu ya hali ya
juu sana,alikuwa na memory ya hali ya juu sana lakini bado alikuwa analalamika
kuhusu kumbukumbu(memory). Lakini sisi kumbukumbu zetu ni dhaifu na ni ndogo sana na mara nyingine hatuwez
kukumbuka hata namba za simu.
Katika miaka ya nyuma tulikuwa
tunaweza hilo.Lakini teknolojia imetufanya
tuwe wazembe.
Imamu Shafii na kumbukumbu yake
ya hali ya juu (powerful memory) lakini alikuwa bado analalamika. Na anasema
nilikuwa nalalamika kwa Wakii ibn Jarrah kuhusu kumbukumbu yangu na akaniongoza
akisema” acha kufanya dhambi, kuwa mbali na dhambi, chochote chenye dhambi kaa
nacho mbali kwasababu ujuzi ni mwanga(light) ambao Allah amewapa na haupatikani
pamoja na mtu anayefanya dhambi”.
Tujitahidi kuacha kufanya dhambi
ili Allah atuongezee kumbukumbu na ujuzi.
0 comments:
Post a Comment