Mitazamo ya Wanafalsafa juu ya Qadar
Wanafalsafa waliojaribu kukitegua kitendawili cha Qudra ni wengi sana na wanahitlafiana katika vipengele vingi. Hata hivyo kimsingi hoja za wanafalasafa hao zimegawanyika katika makundi makuu mawili.
Kundi la kwanza linasema :
kuwa binadamu anayo mamlaka kamili juu ya mwenendo wote wa maisha yake na kwamba ingawa Mwenyezi Mungu anajua kila kitu lakini anajua tu baada ya tukio kutokea na siyo kabla. Wengine wanasema Mungu hayupo na hivyo binadamu ni mdhibiti wa kila kitu.
Kundi la pili linasema:
Mwenyezi Mungu ana mamlaka kamili juu ya maisha yetu na halitokei jambo ila limeidhinishwa naye. Jitihada zote anazozifanya binadamu ni za kutupa nguvu bure kwani kila kinachotokea binadamu hana hiari yoyote. Wengine wanasema mwenendo mzima wa maisha ya kila binadamu umekwishapangwa lakini binadamu anaweza kujua kila alichopangiwa kama atajua namna ya kusoma mwenendo wa nyota yake au kitanga chake (n.k) lakini hataweza kubadili hata akijua kabla na wengine wanasema anaweza kubadili nuksi kuwa bahati akitoa kafara fulani n.k.
Maana ya neno Qudra
Kwa bahati mbaya mara nyingi hutokea utatanishi mkubwa sana juu ya maana ya Kudra hasa kwa watu wanaotegemea tafsiri ya Kiingereza ya neno hilo. Katika lugha hiyo Kudra hutafsiriwa kama "pre-destination" au "predetermination". Kitaalamu si makosa kuitafsiri Kudra kuwa ni "predestination". Kwa upande mmoja tafsiri hiyo ni sahihi. Lakini tatizo la tafsiri hiyo ni kuwa neno "predestination" katika lugha ya Kiingereza limebeba pia dhana ya kukata tamaa na moyo wa kuyandaa mambo yaende yendavyo (fatalism). Na hilo limewapelekea baadhi ya wanazuoni wa Kimagharibi wadai kuwa Uislamu unawafundisha wafuasi wake wawe na tabia hiyo ya kukata tamaa.
0 comments:
Post a Comment